1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Solskjaer awasiliana na Ferguson kuhusu changamoto za Man U

Sekione Kitojo
21 Desemba 2018

Ole Gunnar Solskjaer  amesema kwamba  tayari  amekuwa  akichukua  ushauri  kutoka kocha  wa  zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson tangu  kuchukua  jukumu  la kiti  moto  katika  klabu  hiyo  ya Old Trafford.

https://p.dw.com/p/3AUCI
Europapokal Finale Manchester United - Bayern München 1999
Mshambuliaji wa Man Utd Ole Gunnar Solskjaer akifunga bao la ushindi dhidi ya Bayern Munich 1999 katika fainali ya champions LeaguePicha: Imago
Bildergalerie Sir Alex Ferguson
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex FergusonPicha: PAUL ELLIS/AFP/Getty Images

Ole Gunnar Solskjaer  ambaye  ni  raia  wa  Norway  anachukua  nafasi  ya  Jose  Mourinho , ambaye  alifutwa  kazi siku  ya  Jumanne, akitia  saini  makubaliano  ya  mkataba  wa  muda mfupi  hadi  mwisho  wa  msimu  huu  akiwa   kama  kocha  mlenzi.

Solskjaer alikutana  na  kikosi  cha  Man United  kwa  mara  ya  kwanza  siku  ya  Alhamis  na katika  mkutano  wake  wa  kwanza  na  waandishi  habari  siku  ya  Ijumaa, alifichua kwamba Ferguson  tayari  amekuwa  katika  sikio  lake.

"Amenishawishi  katika  kila  kitu," Solksjaer alisema.

"Amekuwa kioo changu, wakati  wote  tangu  nilipoumia  mwaka  2003 takriban, nilikuwa naweka  kumbukumbu  juu  kile  anachokifanya  katika , maeneo  tofauti , na  bila  shaka tayari  nimewasiliana  nae  kwasababu  hakuna  mtu  mwingine  anaweza  kunipa  ushauri bora kuliko  yeye."

Mshambuliaji  huyo  wa  zamani  wa  United, ambaye  alipachika  wavuni  bao  la  ushindi katika  fainali  ya  kombe  la  vilabu  la  Champions League  mwaka  1999,  amesema atakuwa  na mchango  katika  malengo  ya  uhamisho wa  wachezaji  katika  dirisha  la uhamisho  la  mwezi  Januari.

Bildergalerie Sir Alex Ferguson
Sir Alex Ferguson akishikilia taji la Premier League nchini EnglandPicha: imago/BPI

Wakati  United  ikiwa  katika  nafasi  ya  sita   katika  Premier League, pointi 19 nyuma  ya viongozi  wa  li