Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amejiuzulu wadhifa huo. Ndugai amesema amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ya kujiuzulu nafasi ya Spika na ameweka wazi kuwa uamuzi huo ameufanya kwa hiari. Watanzania wamepokea vipi uamuzi wa Ndugai kujiuzulu?