Starmer kuwasili Poland baada ya ziara yake nchini Ukraine
17 Januari 2025Matangazo
Ofisi ya Starmer ya Downing Street imesema Uingereza na Poland zinatazamiwa kuyajadili makubaliano mapya ya ulinzi na usalama. Starmer amesema Uingereza na Poland ni washirika wa muda mrefu na ushirikiano wao utadumishwa hadi vizazi vijavyo.
Soma pia:Uingereza yaahidi kuihakikishia Ukraine usalama
Haya yanajiri siku moja baada ya Starmer kufanya ziara yake ya kwanza mjini Kiev ambapo kiongozi huyo ameahidi kushirikiana na Ukraine ili kutoa dhamana za kiusalama.