Steinmeier kuboresha ushirikiano na Afrika
20 Novemba 2015Steinmeier amesema alipoanza ziara yake barani Afrika kwamba analichukulia bara la hilo kwa umuhimu wa juu katika kipindi chake cha wadhifa huo kama waziri wa mambo ya kigeni. Mwanzoni mwa ziara yake amelitembelea taifa lililokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu Msumbiji.
Yalikuwa ni mapokezi mazuri ya aina yake. Na baada ya shambulio la kigaidi mjini Paris waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani alikuwa anataka kutoa ishara maalum. "Kwangu mimi ina maana na kuchukulia kwa dhati maneno yetu, kwamba tunalichukukia kwa dhati suala la bara la Afrika kutaka mabadiliko na kuimarisha hali iliyopo,“ alisema Steinmeier. "Hii ina maana tunaliangalia bara la Afrika kwa dhati. Katika maeneo kadhaa, jamii ya Wajerumani iko pamoja na bara hili la Afrika katika hatari na mizozo."
Makampuni ya Ujerumani yataka kuwekeza
Masuala ya kisiasa bila shaka yamejadiliwa. Kwa uwazi lakini pia kwa njia ya kidiplomasia. Lakini ni wazi pia kwamba suala la uchumi liko mbele zaidi. Pamoja na kwamba shauku kubwa ya kuwapo kwa hazina kubwa ya gesi ya ardhini katika pwani ya kaskazini nchini Msumbiji, bei ya mafuta na gesi imeporomoka.
Bado hatua ya uchimbaji gesi imo katika awamu ya mipango, kwa makampuni makubwa kuweza kuchima gesi hiyo. Na makampuni ya Ujerumani yanataka nayo kujihusisha katika uchimbaji huo. Sabine Dall'Omo ni mwanamke pekee katika ujumbe wa masuala ya kiuchumi katika msafara huo wa waziri wa mambo ya kigeni Steinmeier.
Ni mkurugenzi wa kampuni ya Siemens nchini Afrika kusini. Anasema suala muhimu ni ukuaji endelevu wa uchumi wa Msumbiji, ili kuweza kuwanufaisha wananchi wengi zaidi. "Hii haina maana kwamba makampuni ya kimataifa kuja Msumbiji na kuchukua maliasili na kuiacha nchi kama ilivyo, badala yake ukuaji wa uchumi pia usaidie jamii."
Bara la Afrika lenye fursa, ndio picha inayopaswa kuonekana. Msumbiji kama kawaida ni nchi yenye matatizo, karibu nusu ya watu wazima hawajui kusoma na kuandika, mapambano ya silaha baina ya chama tawala cha Frelimo na waasi wa Renamo, ambao wako katika eneo masikini la kaskazini, yanazuwia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Waziri Steinmeier anakutana na rais wa Zambia Edgar Lungu. Zambia ni moja kati ya nchi zinazozalisha kwa wingi madini ya shaba. Uchumi wa nchi hiyo yenye wakaazi karibu milioni 16 kwa muda mrefu umekuwa ukiendelea kukua. Kuporomoka hivi karibuni kwa bei ya shaba duniani kunaiweka Zambia katika hali ngumu. Ziara ya Steinmeier pia itamfikisha nchini Uganda na Tanzania.
Mwandishi: Ingo Mannteufel
Mhariri: Josephat Charo