1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan,Sudan Kusini kujaribu karata ya mwisho

Admin.WagnerD25 Septemba 2012

Viongozi wa Sudan na Sudan Kusini leo watajaribu kwa mara nyingine kufikia makubaliano kuhusu masuala ya ulinzi kwenye eneo la mpaka baada ya kushindwa kuafikiana juu ya suala hilo katika mazungumzo siku mbili zilopita.

https://p.dw.com/p/16DhR
Bashir na Kiir
Bashir na KiirPicha: picture-alliance/dpa

Maafisa wanaofuatilia mazungumzo hayo wanasema kuwa pande zote mbili zinakataa kwamba kuna hatua ya maendeleo iliopatikana kwenye mazungumzo hayo.

Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan na mwenziwe Salva Kiir wa Sudan Kusini wamekuwa na mkutano nchini Ethiopia tangu Jumapili iliyopita kwa matumaini ya kukamilisha mazungumzo ya amani baada ya kunusurika kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa mara nyingine mwezi Aprili mwaka huu.

Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan akiwa Sudan Kusini na Rais Salva Kiir
Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan akiwa Sudan Kusini na Rais Salva KiirPicha: AP

Umoja wa Afrika umekuwa katika juhudi za kuhakikisha kunaundwa eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi katika mpaka wa nchi hizo mbili, ili kuanza usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kupitia Sudan jambo ambalo litainua uchumi wa mataifa yote mawili.

Shinikizo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Nchi hizo ziko chini ya shinikizo baada ya muda uliowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa majirani hao kumaliza tofauti zao kumalizika Jumamosi iliyopita, ingawa muda huo uliongezwa kimya kimya hadi Alhamis wiki hii (27.9.2012) wakati mapatanishi wa Umoja wa Afrika katika mzozo huo Thabo Mbeki atakapotoa ripoti kama makubaliano yamefikiwa.

Bashir na Kiir walipanga mkutano wa kilele wa siku moja lakini hadi walishindwa kufikia muafaka katika vikao virefu walivyofanya kujadili taarifa kuhusu pendekezo la ramani lililotolewa na Umoja wa Afrika kuhusu eneo maalumu ambalo haliruhusiwi shughuli za kijeshi.

Sudan inataka ipewe eneo zaidi la kilometa 23 nje ya ramani hiyo, wakati Sudan Kusini yenyewe imekubaliana nayo ramani hiyo bila kikwazo. Sudan inasema kuwa kuwa ina matumaini kuwa Bashiri na Kiir watakamilisha mazungumzo hayo hii leo kwa mafanikio.

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaPicha: AP

"Viongozi hao watajidili sualahilo hao kesho. Tunatarajia masulala yote yatapatiwa ufumbuzi kwa mafanikio" alisema El-Obeid Morawah, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan akiwaambia waandishi wa habari masaa mawili baada ya Rais Bashir na Kiir kukutana jana (24.9.2012).

Mashaka juu ya mazungumzo hayo

Ujumbe wa mataifa hayo kwenye mazungumzo unaonekana kuwa na mshaka. " Tumekuwa tukikabiliwa na matatizo wakati wa mazungumzo ya marais hao. Hatujaweza kutatua tatizo hili hadi sasa lakini kesho kikao cha mwisho kitafanyika" alisema Atif Keir, msemaji wa ujumbe wa Sudan Kusini unaohudhuria mazungumzo hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

ARCHIV - Südafrikas Thabo Mbeki, Mpatanishi wa Umoja wa Afrika kwenye mzozo wa Sudan mbili.
Thabo Mbeki, mapatanishi wa Umoja wa Afrika kwenye mzozo wa Sudan mbili.Picha: picture-alliance/dpa

Keir anasema kuwa mazungumzo ya leo yatakuwa na mafanikio kama tu Sudan itakubaliana na mpango wa amani wa Umoja wa Afrika. Tangu kuzuka kwa mapigano makali ya mwezi Aprili mwaka huu ambayo ama nusura yazushe vita kwa mara nyingine, matifa hayo yamefanya mazungumzo ya mani mara kadhaa. Mwezi Agosti mwaka huu zilikubaliana kuanza tena usafirishaji wa mafuta. Hata hivyo mazungumzo hayo hayajaonyesha dalili ya kupatikana muafaka baina ya nchi hizo.

Mwandishi: Stumai George/Reuters/AP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman