1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden, Denmark wachoma tena nakala za Qur'an

31 Julai 2023

Nakala za kitabu kitakatifu kwa Waislamu, Qur'an, zimechomwa moto leo nchini Sweden na Denmark ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya aina hiyo yanayotishia kuongeza mivutano kati ya nchi hizo na ulimwengu wa Kiislamu.

https://p.dw.com/p/4Ubd5
Libanon Beirut | Proteste gegen Koran-Schändung in Schweden
Picha: Bilal Hussein/AP/picture alliance

Kwenye mji mkuu wa Sweden, Stockholm, wanaume wawili waliotambulishwa kwa majina ya Salwan Momika na Salwan Najem walionekana wakiikanyaga nakala ya Qur'an, kuchana kurasa za kitabu hicho na kukitia moto mbele ya majengo ya bunge la nchi hiyo. 

Nchini Denmark, waandamanaji wanawaopinga Waislamu wameichoma nakala ya Qur'an mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Copenhagen.

Soma zaidi: Uturuki yaitaka Denmark kuchukua hatua uchomaji Quran

Wairaqi waandamana tena baada ya tukio la kuchoma kwa Qur'an

Matukio ya aina hiyo yameshuhudiwa mara kadhaa katika miezi ya karibuni na yamezusha ghadhabu miongoni mwa mataifa yenye Waislamu wengi. 

Mataifa hayo yamezilaumu serikali za Sweden na Denmark kwa kutochukuwa hatua kuzuia kile kinachotajwa kuwa matendo ya kuukashifu Uislamu na kunajisi kitabu kitakatifu cha Quran. 

Kufuatia matukio ya leo, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) imetisha kikao cha dharura cha ngazi ya mawaziri kushughulikia suala hilo.