1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Marekani kutafakari amani na Korea Kaskazini

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBS0

Rais George W Bush amesema Marekani itatafakari juu ya kuwa na makubaliano ya amani na Korea Kaskazini iwapo nchi hiyo itawacha kabisa nia yake ya kumiliki silaha za nyuklia.

Bush ameyasema hayo mjini Sydney kabla ya kuanza mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Asia na Pacifc.

Wakati huo huo mjumbe wa Marekani katika maswala ya nyuklia ya Korea Kaskazini naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Christopher Hill amesema mjini Sydney kwamba watalaamu wa nyuklia kutoka China, Urusi na Marekani watazuru Korea Kaskazini kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 15 mwezi ujao kwa mualiko wa Pyongyang kwenda kushuhudia kufungwa kwa vinu vitatu vya nyuklia vilivyokuwa vinajadiliwa katika mazungumzo ya pande sita.

Washington inalaumiwa kwa kulipuuza bara la Asia na kulekea zaidi katika maswala ya Irak.