Chama cha Christian Democratic Union CDU chapata pigo katika chaguzi za majimbo mawili muhimu kuelekea uchaguzi wa bunge mwezi Septemba/ Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya waandamanaji Myanmar huku sheria ya kijeshi ikitangazwa katika vitongoji vya Yangon/Na Kenya haitohudhuria kesi kuhusu mpaka na Somalia inayoanza kusikilizwa leo na mahakama ya kimataifa ya haki ICJ mjini The Hague