18 Machi 2019
Matangazo
Shughuli zaanza tena chini ya ulinzi mkali katika mji wa Christchurch nchini New Zealand, kufuatia shambulizi kubwa la kigaidi Ijumaa iliyopita, Ethiopia yasema uchunguzi wa awali waonyesha kufanana kabisa kwa sababu za ajali ya ndege ya nchi hiyo na ile ya Lion Air iliyotokea Oktoba iliyopita, na kimbunga Idai chauwa watu zaidi ya 100 katika mataifa ya Msumbiji na Zimbabwe.