1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tahmini ya ushindi wa Zuma na athari zake kwa siasa za ANC

Siraj Kalyango19 Desemba 2007

Mbeki na Zuma lazima waondoe tofauti zao

https://p.dw.com/p/CdpY
Rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki, kushoto, na kiongozi mpya wa ANC Jacob Zuma,wakisimama wima wakati wimbo wa taifa ukipigwa katika mkutano mkuu wa chama ambapo Zuma alimshinda Mbeki kukiongoza chama tawalaPicha: AP

Nchini Afrika kusini baado kinachozungumzwa ni ushindi wa Bw Jacob Zuma na wafuasi wake katika uongozi wa chama tawala cha ANC.

Pamoja na ushindi wa Zuma dhidi ya Rais Thabo Mbeki katika kuwania uongozi wa chama hicho kuwatia wasi wasi baadhi ya watu wa nje na ndani ya nchi hiyo wakihofia huenda akipata nafasi ya kuwa rais ajae wa nchi hiyo atabadili sera za mtangulizi wake, lakini wachambuzi wanaungama kwamba zoezi la uchaguzi katika ANC lilikua la demokrasia ya hali ya juu licha ya mvutano uliotokea.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Harald Pakendorf, amenukuliwa kusema kwa kuwa uongozi umegombaniwa-hilo ni dhahirisho tosha la demokrasia.

Hata hivyo ameonya kuwa ikiwa Zuma na kiongozi wa nchi ,Thabo Mbeki, hawatamaliza tofauti zao, huenda Afrika Kusini itakabiliwa na matatizo sio tu ya kisiasa lakini pia ya kiuchumi hadi uchaguzi mkuu wa mwaka 2009.

Akifafanua kauli yake mchambuzi huyo, ameeleza kuwa mvutano ndani ya chama hicho ANC utakizuia kusonga mbele kama chama kimoja.Na hilo litakuwa na athari za kiuchumi,kwani wawekezaji hawataki vurugu.

Pakendof ameongeza kuwa huku mabadiliko ya kiuchumi yanategemewa chini ya Zuma, ambae sasa njia ya kwenda Ikulu mwaka wa 2009 ikiwa imeanza kuonekana, mwelekeo huo umanza kudhihirika katika utawala wa Mbeki kama mkuu wa chama cha ANC.

Serikali,amefafanua, imesha anza kuchangia zaidi uchumi, na ule unaoweza kuitwa mwelekeo wa kushoto tayari umesha anza.

Ingawa Zuma amesisitizia haja ya kuwepo kwa ajira,lakini juhudi kuelekea hilo zimesha chukuliwa.

Mchambuzi mwingine, Max du Preez, anabaini kuwa huenda hakutakuwa na mageuzi zaidi.

Akilihutubia taifa mwishoni mwa juma-rais Mbeki amewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ANC wa 52 kuwa, viwango vya umaskini vilishuka tangu mwaka wa 1994, ambapo ilikuwa alama ya kuingia kwa demokrasia nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo amekiri kuwa japo kuna maenedeleo fulani katika kupunguza umaskani lakini pia,pato la matajiri nalo linaongezeka haraka kusababisha pengo kati ya maskini na matajiri kuzidi kupanuka.Na idadi ya vijana wasio na kazi nayo inaendelea kupanga.

Wachunguzi fulani,miongoni mwao ni mwanafilosofia wa masuala ya kisiasa-Willie Esterhuyse, wanasema wafuasi wa Zuma wanamuona kama muokozi wao,ambae atachapuza mageuzi ya kijamii pamoja na kiuchumi.

Lakini yeye mchambuzi wa siasa katika taasisi ya Demokrasia ya Afrika kusini, Steven Friedman, hakubaliani na hoja hiyo akisema kuwa uungaji wa Zuma sio wa ukombozi bali ni uasi dhidi ya mbeki na aina fulani ya uongozi wa chama.

Kuna nadharia eti Mbeki anaweza akachochea mamlaka ya taifa ya mashataka kuhsu aidha kumpleka mahakamani Zuma.Du Preez anasema ikiwa Zuma atashitakiwa –hatua hiyo inaweza ikazusha fujo.

Halafu kuna habari eti Zuma atataka kupigwa kura ya kutokuwa na imani na Mbeki ili kuchapuza tarehe ya uchaguzi mkuu.Hilo limekataliwa na mchambuzi Friedman.Anatetea msimamo wake kuwa ili kufanikiwa na hilo Zuma anahitaji kupata kura 201 za wanachama 294 ambao ni wabunge ili kuweza kukubali. Hii inamaan kuwa zaidi ya asili mia 70 ya ANC itakuwa imepiga kura dhidi ya Mbeki.Friedman asema hajui kama hilo lawezekana.