Takribani watu 7 wauawa kwenye shambulizi nchini Mali
16 Desemba 2024Ofisi ya Dayosisi ya mkoa wa Mopti nchini humo imeiambia AFP kwamba "shambulizi la kigaidi" limekilenga kijiji cha Segue na ndugu mmoja wa kasisi pamoja na wanaume wengine 6 wameuawa. Taarifa hiyo ya kanisa imesema shambulizi hilo pia limesababisha "uharibifu mkubwa wa mali".
Chanzo kingine ambacho ni shirika la kiraia limesema limeshtushwa na mashambulizi kwenye vijiji viwili vya Segue na Sonfounou na kwamba idadi ya waliopoteza maisha imeongeza na kufikia 9 ambapo saba ni kwenye kijiji cha Segeu na wawili huko Sonfounou.
Mali imekuwa ikipambana na mizozo ya kisiasa, kiusalama na kiucuumi na imeshuhudia hujuma za makundi hasimu ya itikadi kali za kiislamu tangu mwaka 2012. Inakabiliwa pia na uasi wa wanaotaka kujitenga upande wake wa kaskazini ambao sehemu kubwa ni jangwa.