1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Taliban yasema watu 46 wauawa kwenye mashambulio ya Pakistan

25 Desemba 2024

Afisa wa serikali ya Taliban amesema watu 46 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa kutokana na mashambulio ya anga yaliyofanywa na Pakistan

https://p.dw.com/p/4oZZK
ARCHIV | Pakistan | Soldaten nach Explosion
Picha: Fahad Pervez/PPI Photo/Newscom/IMAGO

Mashambulio hayo ya anga yalifanywa na Pakistan mashariki mwa Afghanistan. Hamdullah Fitrat, ameeleza kuwa watu wengine sita waliuawa pia katika hujuma hizo.

Mashambulio hayo yamefanyika siku moja baada ya maafisa wa usalama wa Pakistan, kuliambia shirika la habari la AP, kwamba operesheni hiyo ililenga kukiteketeza kituo cha mafunzo na kuwaua waasi katika jimbo la Paktika nchini Afghanistan.

Mpaka sasa, Pakistan haijasema chochote juu ya mashambulio hayo licha ya kutoa habari juu ya kuuliwa waasi 13 kwenye wilaya ya Waziristan kusini, iliyopo kwenye jimbo la mashariki mwa Afghanistan.