Tamasha la amani ambalo limekuwa likikosolewa mara kadhaa na miungano ya vijana kutokana na kuendelea kuchafuka kwa hali ya usalama kote hapa mashariki mwa Jamhuri a Kidemokrasia ya Kongo, limewaleta pamoja wasanii kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika katika lengo la kuwahimiza raia kuhusu amani ambayo wengi wao wamepoteza matumaini ya kuipata.