Tanzania: Dr.Steven Ulimboka arejea nchini baada ya kutibiwa Afrika Kusini
13 Agosti 2012Matangazo
Daktari Steven Ulimboka ambaye aliongoza mgomo wa madaktari kabla ya kupigwa vibaya na watu wasiojulikana, na kulazimika kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu, amerejea jana akiwa na afya njema na kusema yuko tayari kuanza tena kazi. Iddi Ssessanga amezungumza na Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Edwin Chitaga, ili kujua mengi zaidi kuhusiana na kurejea kwa Dk. Ulimboka na kwanza alianza kumuelezea kuhusiana na hali ya sasa ya Daktari huyo.
(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni)
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman