Serikali ya Tanzania imetangaza kuazisha operesheni kali ya kuwasaka wahamiaji haramu ikiwemo wale wanaofanyakazi kinyume na sheria. Hatua hiyo iliyotangazwa na wizara ya mambo ya ndani ni sehemu ya kukabilia na vitendo vya uhalifu na kuwawezesha Watanzania kupata ajira chache zilizoko.