TEHERAN: Rais wa Venezuela ziarani Iran
30 Julai 2006Matangazo
Rais Hugo Chavez wa Venezuela na rais mwenzake wa Iran,Mahmoud Ahmedinejad wamekutana mjini Teheran na wameahidi kusaidiana.Chavez,anaejulikana kuwa ni mkosoaji wa serikali ya Marekani yupo Teheran kwa ziara ya siku mbili.Marais hao wawili wamesema wanahisi kama ni ndugu.Mkuu wa kidini wa Iran,Ayatollah Al Khamanei ameituhumu Marekani kuwa inapigania kueneza ushawishi wa Kimarekani katika eneo zima la Mashariki ya Kati.Kwa maneno yake,”Mradi huo umeshindwa kufanikiwa kwa sababu ya upinzani wa kishujaa wa Hezbollah nchini Lebanon.”