Miaka tisa iliyopita shirika la kimataifa linalosimamia mawasiliano ya simu, ITU, liliiweka tarehe 17 ya mwezi wa Juni kuwa siku ya mataifa yote ya Afrika kuhamia katika mfumo wa digitali lakini nchi nyingi zimejikuta katika hali ya kutokuwa tayari.
https://p.dw.com/p/1FpLH
Matangazo
Nyingi ya nchi za kanda ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hazikujiandaa kuanza mfumo huo. Hata nchi ambazo kiuchumi ziko imara na mfumo wake wa mawasiliano ya televisheni kuonekana kuwa bora kama Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zimekabiliwa na matatizo.