1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaVanuatu

Tetemeko la ardhi lawaua watu 14 kisiwa cha Vanuatu

18 Desemba 2024

Tetemeko kubwa la ardhi lililokitikisa kisiwa cha bahari ya Pasifiki cha Vanuatu limesababisha vifo vya watu 14, huku juhudi za kuwatafuta manusura bado zinaendelea.

https://p.dw.com/p/4oHSe
Vanuatu, Port Vila | Tetemeko la ardhi
Athari za tetemeko la ardhi kwenye kisiwa cha bahari ya Pasifiki cha Vanuatu.Picha: AFP/Getty Images

Takwimu hizo  zimetolewa na serikali ya nchi hiyo usiku wa kuamkia leo Jumatano huku kukiwa na wasiwasi wa kuongezeka kwa idadi ya vifo.

Kwenye taarifa yake, serikali imesema idadi hiyo ya watu 14 inajumuisha 4 waliokufa kwenye hospitali ya mji mkuu, Port Vila, 6 kwenye maporomoko ya udongo na wengine 4 kwenye jengo lililoporomoka kutokana na mtetemo.

Tetemeko hilo la ukubwa wa 7.3 kwenye kipimo cha Richter lillotokea Jumanne mchana kwa saa za Vanuatu.

Vikosi vya uokoaji bado vinaendelea kuwatafuta manusura wa janga hilo la asili ambalo limeangusha majumba, kusababisha nyufa kwenye kuta na madirisha, kuharibu madaraja na kuzusha maporomoko ya ardhi kwenye kisiwa hicho cha wakaazi 320,000.

Kwenye jumba moja la ghorofa lililiporomoka katikati mwa mji mkuu, sauti za watu zilikuwa bado zinasikikika kutoka ndani ya kifusi hadi majira ya usiku.