Timu 16 zasubiri droo ya mtoano
8 Desemba 2016Timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu katika kila kundi zimejikatia tikiti ya kucheza katika hatua ya mtoano ya dimba la Europa League.
Droo ya kupanga michuano ya hatua ya mtoano ya timu kumi na sita itafanyika Jumatatu Decemba 12 mjini Nyon, Uswiwi.Timu zilizofuzu kutoka kundi A ni Arsenal wakiwa vinara wa kundi na Paris Saint Germain katika nafasi ya pili. Katika Kundi B kuna vinara Napoli na Benfica katika nafasi ya pili.
Kundi C wamefuzu vigogo Barcelona wakifuatwa na Manchester City wakati Kundi D lina vinara Atletico Madrid na Bayern Munich. Katika Kundi E Monaco wamefuzu kama vinara wakifuatwa na Wajerumani Bayer Leverkusen, na kundi F lina vigogo wa Ujerumani Borussia Dortmund na miamba wa Uhispania Real Madrid katika nafasi ya pili.
Leicester na Porto wamefuzu kutoa kundi G huku Juventus na Sevilla wakiwa wamefuzu katika kundi la mwisho kundi H
Mwandishi: Bruce Amani/DW
Mhariri: Daniel Gakuba