Togo wachaguwa wabunge baada ya mageuzi tata ya katiba
30 Aprili 2024Matangazo
Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa vituo vya kura vilifungwa mwendo wa saa 12:00 jioni ya Jumatatu (Aprili 29) na baada ya hapo kura zikaanza kuhesabiwa.
Taarifa ya tume ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa huenda matokeo ya awali yangelianza kutolewa jioni hiyo hiyo.
Soma zaidi: Togo yapiga kura ya wabunge baada ya mageuzi ya kikatiba
Uchaguzi huo ulikuwa wa kuwachagua wabunge 113 na pia kwa mara ya kwanza, makamu wakuu wa mikoa 179 katika wilaya tano, ambao pamoja na madiwani watachagua baraza jipya la seneti.
Kulingana na chama tawala cha Gnassingbe, UNIR, hatua hiyo inaifanya Togo kuwa na uwakilishi zaidi, lakini vyama vya upinzani viliwahamasisha wafuasi kupiga kura dhidi ya kile walichokitaja kuwa mapinduzi ya kitaasisi.