Trump amemteua Kash Patel kama mkurugenzi mpya wa FBI
1 Desemba 2024Matangazo
Katika taarifa aliyoichapisha katika mtandao wa kijamii, Trump alimuelezea Patel kama "wakili mahiri, mpelelezi na mtoa kipaumbele katika maslahi ya Marekani. Patel amefanya kazi katika Kamati ya Intelijensia ya Bunge la Marekani, ambapo alikuwa na wajibu muhimu katika uchunguzi wa madai ya Urusi katika kuuingilia uchagui wa rais wa 2016. Patel, anayejulikana kwa utiifu wake thabiti kwa Trump, alihudumu katika majukumu muhimu wakati wa utawala wa kwanza wa Trump, ikiwa ni pamoja na kitengo cha kusimamia kukabiliana na ugaidi katika Baraza la Usalama la Taifa na baadaye akihudumu kama mkuu wa wafanyakazi katika Idara ya Ulinzi.