1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema Zelensky ana nia ya kumaliza vita

8 Desemba 2024

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ana nia ya kuwa na makubaliano ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine baada ya kukutana nae mjini Paris.

https://p.dw.com/p/4nt1a
Ufaransa Paris 2024 | Macron Trump na Zelensky
Rais mteule wa Marekani Donald Trump, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakiwa katika kasri la Elysee Picha: Sarah Meyssonnier/POOL/AFP/Getty Images

Katika ukurasa wake wa kijamii Trump aliandika kwamba Zelensky anataka makubaliano na kusitisha vita, akisisitiza kuwa lazima pawepo na usitishwaji wa mapigano wa haraka na mazungumzo yanapaswa kuanza. 

Trump amesema maisha ya wengi yameshaangamia na iwapo hatua za haraka hazitochukuliwa mzozo unaweza kutanuka na kuwa mbaya zaidi. 

Scholz: Ninao mkakati wa kuisaidia Ukraine na Trump

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi hao wawili katika kasri la Elysee jana Jumamosi, ikiwa ni takriban miaka mitatu tangu Moscow ilipoivamia kijeshi Kiev na ikiwa ni wiki chache kabla ya Trump kuapishwa rasmi madarakani Januari 20.