1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kujiunga na viongozi wengine kuzungumzia Lebanon

Sekione Kitojo
8 Agosti 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amesema atajiunga na mkutano kwa njia  ya simu pamoja na rais wa Lebanon na viongozi wengine wa  dunia siku ya Jumapili kujadili msaada kwa Lebanon kutokana na mripuko uliotokea mjini Beirut

https://p.dw.com/p/3geBo
Still Beirut: Popular spots reduced to rubble in Lebanese capital
Eneo la maafa ya mripuko wa kemikali mjini BeirutPicha: DW

Trump alisema kupitia Twitter kuwa  alizungumza  binafsi katika  nyakati tofauti  na  rais wa Lebanon  Michel Aoun na rais wa Ufaransa  Emmanuel  Macron, ambae pia  atajiunga na  mazungumzo hayo ya simu. Alisema  amemwambia Aoun kuwa  ndege  kubwa   tatu za Marekani  zimo  njiani kwenda  Lebanon  kupeleka  madawa, chakula, maji na madaktari.

USA I Donald Trump
Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: picture-alliance/dpa/newscom/UPI/K. Dietsch

Trump  na  Macron walizungumza  kwa simu  na  walieleza masikitiko  yao  makubwa  kutokana na  upotevu wa maisha  na uharibifu  mjini  Beirut, msemaji  wa  Ikulu  ya Marekani Judd Deere alisema katika  taarifa.

Rais wa Lebanon  hata  hivyo  amekataa uchunguzi wa kimataifa  kuhusiana  na  maafa ya mripuko mjini Beirut, akisema  kombora  ama  uzembe unaweza  kuwa  chanzo cha mripuko huo wakati waokoaji wanatafuta bila kuchoka watu walionusurika.

Lengo la  mashambulizi ya wananchi

Tabaka la viongozi lililojichimbia katika  utawala wa nchi hiyo limekuwa lengo la  mashambulizi  kwa mara nyingine  tena tangu mripuko  huo kutokea  siku  ya  Jumanne, ambao umewauwa  kiasi  watu 154 na kuharibu sehemu  kubwa  ya  mji huo mkuu.

Libanon, Beirut: Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) akitembelea eneo la maafa mjini BeirutPicha: picture-alliance/dpa/AP/T. Camus

Ufichuaji kwamba  shehena kubwa  ya  kemikali hatari ya  aminia nitrate ilikuwa  kwa  miaka  kadhaa  katika bohari katikati ya mji  mkuu  Beirut umekuwa ni ushahidi  wa  kushitua kwa wengi  wa watu wa Lebanon kuhusiana na kuoza kwa  kitovu cha  mfumo  wao  wa  kisiasa.

Wakati  huo  huo  waraka  mpya  uliopatikana  unaeleza kuwa kwa karibu mara 10 katika  miaka  sita iliyopita maafisa  kutoka  idara ya  forodha ya Lebanon, jeshi, idara ya usalama na  mahakama  walieleza wasi wasi wao  kuwa shehena  hiyo kubwa  ya  kemikali zinazoweza  kuripuka zimewekwa bila kuzingatia  usalama  katika  bandari katikati ya Beirut.