Tshisekedi ataka kukutana na Kabila
9 Juni 2016Matangazo
Upinzani umefanya "Mkutano wa Ubelgiji" wenye lengo la kushinikiza uchaguzi mkuu wa taifa lao ufanyike kama ulivyopangwa mwishoni mwa mwaka huu. Zaidi ya wajumbe 200 kutoka katika karibu vyama vyote vya upinzani nchini humo wanashiriki mkutano huo. Kutoka mjini Brussels kunakofanyika mkutano huo, DW imezungumza na mmoja wa washiriki, Mbunge Muhindo Nzangi, na kwanza anaelezea ni yapi wameyafikia mpaka muda huu.