1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya Umoja wa mataifa iya kusimamia amani nchini Burundi imekamilisha shughuli zake

23 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEia

Kamisheni ya umoja wa mataifa iliyokua ikisimamia kipindi cha mpito cha miaka mitano kuelekea demokrasia nchini Burundi iliitisha mkutano wake wa mwisho jana mjini Bujumbura.Kamisheni hiyo imesifu kile ilichokiita „mfano adimu wa ufumbuzi wa amani wa mzozo wa ndani barani Afrika.Kipindi cha mpito kimemalizika kwa kuchaguliwa rais mpya,Pierre Nkurunziza na mabaraza yote mawili,Senet na bunge ijumaa iliyopita.Mwenyekiti wa kamisheni ya umoja wa mataifa bibi Carolyn McAskie na Umoja wa Afrika wamewatolea mwito wafadhili wa kimataifa wazidi kuiunga mkono serikali mpya ya Burundi.Bibi McAskie amesema Umoja wa mataifa unajishughulisha hivi sasa kubuni taasisi itakayokua na uwezo wa kuishauri na kuisadia serikali mpya.“Tukimuacha Nkurunziza baada ya kuchaguliwa ,hatofanikiwa.Tunabidi tumsaidie“ amesema kwa upande wake muakilishi maalum wa Umoja wa Afrika Mamadou Bah.