Ubalozi wa Marekani wafungwa Kinshasa kwa hofu za shambulizi
29 Novemba 2018Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa umeendelea kufungwa kwa siku ya nne leo , baada ya Marekani kuonya kuhusiana na uwezekano wa kitisho cha ugaidi dhidi ya ubalozi huo katika jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Raia wa Marekani mjini Kinshasa pamoja na maeneo mengine ya Congo wanatakiwa kuchukua tahadhari na kuwa macho katika hali mbali mbali, ubalozi huo umesema.
Ubalozi huo ulifungwa siku ya Jumatatu. wakati makundi kadhaa ya wanamgambo yanapigana nchini Congo, kwa misingi ya kikabila ama kuhusiana na utajiri wa madini nchini humo, ambapo mara kadhaa wafanyakazi wa nje wa mashirika ya misaada wakikumbana na matatizo katika mzozo huo, si kawaida kwamba Marekani inaweza kukabiliwa na kitisho hicho.