1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Afrika Kusini

22 Aprili 2009

Wastahiki milioni 23 nchini Afrika Kusini leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa nne, ambapo chama kinachotawala ANC kinatarajiwa kushinda tena kwa kura nyingi.

https://p.dw.com/p/HboH
Kiongozi wa ANC Jacob ZumaPicha: AP



Chama cha ANC kitakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa vyama vya upinzani.Uchaguzi wa leo pia unatarajiwa kumpitisha rais wa chama hicho Jacob Zuma kuwa rais wa nchi vilevile.


Chama cha ANC kinatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo mkuu na mgombe urais wa chama hicho Jacob Zuma pia anatazamiwa kupita kwa kura nyingi.

Watu walianza kupiga kura nchinini kote saa moja asubuhi kwenye vituo vya kupigia karibu alfu 20 katika zoezi litakalochukua muda wa saa 14.

Soweto
Mtaa wa SowetoPicha: Jana Genth

Wananchi milioni 23 wanastahiki kupiga kura kuwachagua wabunge mia nne.


Kiongoziwa chamacha ANC aliyefutiwa mashtaka ya rushwa hivi karibuni ameahidi kuyakabili kwa nguvu zote matatizo yanayotokana na umasikini.

Katika kampeni za uchaguzi Zuma aliwasilisha ujumbe wa kuendeleza mafanikio ya demokrasia kwa manufaa ya mamilioni ya watu wake wanaoishi katika umasikini.

Hatahivyo Zuma mwenye umri wa miaka 67 amewahakikishia wapinzani kwamba licha ya chama cha ANC kuthibiti theluthi 2 ya viti vya bungeni,chama hicho hakina mpango wa kubadili katiba.Zuma aliongeza,''Hatutakiuka haki za binadamu na wala hatutavikandamiza vyama vya upinzani na kuvilazimisha kujisalimisha"

Uchaguzi mkuu wa safari hii ni wa kusisimua kutokana nanguvu za vyama vya upinzani kuongezeka.Vyama vya siasa vimetumia kiasi cha Euro milioni 25 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi. Chama cha ANC pekee kimetumia Euro milioni 17.

Macho yote yanaangazia katika chama kipya cha upinzani Congress of the People kilichoundwa hivi karibuni na wanasiasa waliojitoa ANC.

Chama hicho kilichonufaika kwa muda mfupi kutokana na mashtaka ya rushwa yaliyomkabili Jacob Zuma sasa kimepoteza kasi ya hapo awali.

Mgombea urais wake ni askofu Mvume Dandala asiyejukilikana sana . Kuchaguliwa kukiwakilisha chamachake kumewashangaza watu kidogo.

Licha ya kuwasilisha ujumbe wa keleta mabadiliko chama cha Congress of the People hakitarajiwi kukishtua sana chama kiachotawala ANC.Chama hicho kinatazamiwa kupata asilimia 10 ya kura.

Changamoto nyingine kwa chama tawala anc itatoka kwa chama cha DA kinachoongozwa na Helen Zille mwanasiasa mzungu.Chama hicho kilipata asilimia 12 ya kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2004.Lakini kura za maoni zinaonyesha kuwa safari hii kitapata asilimia 10 ya kura.

Chama cha ANC kinatarajiwa kufikia asilimia 60 ya kura.Ni kiwango cha uhakika lakini kinaashiria pungufu kulinganisha na uchaguzi wa hapo awali.

Shughuli za kupiga kura zitamalizika saa tatu usiku za saa afrika kusuini na matokeo hayatajulikana kabla ya ijumaa.

Bunge jipya litakutana wiki mbili baadaye ili kumchagua mkuu wa nchi-rais anaetazamiwa kuwa Jacob Zuma-

Mwandishi:Claus Stäcker/ ZR/A Mtulya

Mhariri:M Abdulrahman