ANC yathibiti kuwa na nguvu kubwa
23 Aprili 2009Matangazo
PRETORIA.
Hesabu za awali katika uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini zinaonesha kuwa chama kinachotawala ANC kipo mbele sana, wakati chama kipya cha upinzani Congress of the People kimeshindwa kupiga hatua kubwa. Kura karibu alfu 23 zimeshahesabiwa kati ya idadi ya milioni 23 zinazotarajiwa.
Chama cha ANC kinaongoza kwa asilimia karibu 60 wakati chama kipya cha upinzani kimefikia asilimia 8 nukta 7 tu.
Na chama kikuu cha upinzani ,Democratic Alliance kipo katika asilimia 26.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba chama kipya cha Cope kilichotarajiwa kuwa changamoto kubwa kwa chama kinachotawala hadi sasa kimeshindwa kukatua sehemu kubwa.