Uchaguzi wa Bunge Apirl na Mei nchini India:
29 Februari 2004Matangazo
NEW DELHI: Nchini India uchaguzi mkuu wa bunge umepangwa kufanyika katikati ya April mpaka katikati ya Mei katika duru nne, ilitangaza tume huru ya uchaguzi. Wapiga kura zaidi ya miliyoni 670 wanatazamiwa kushiriki katika uchaguzi huo wa bunge baina ya April 20 na Mei 10. Kwa kulingana na kura ya maoni chama tawala cha Bharatiya Janata, BJP kingaliko mbele kwa sababau ya kuendelea ustawi wa uchumi pamoja na kule kuongezwa juhudi za mkaribiano kati ya India na hasimu wake mkubwa Pakistan. Kufuatana na ushauri wa chama cha BJP Rais Abdul Kalam aliliuzulu bunge hapo Fabruari na kufungulia njia ya kufanyika uchaguzi mpya. Chama cha BJP kinachoongozwa na Waziri Mkuu Atal Bihari Vajpayee kinatawala tangu mwaka 1999, kikiwa kinaongoza serikali ya mwungano wenye zaidi ya vyama 20.