1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge Burundi wafanyika leo

Josephat Nyiro Charo23 Julai 2010

Upinzani umeugomea uchaguzi huo kama ulivyofanya wakati wa uchaguzi wa rais. Idadi ya wapiga kura waliojitokeza vituoni ni ndogo

https://p.dw.com/p/OTQr
Raia wa Burundi akitumbukiza kura yake katika kituo kimoja cha uchaguziPicha: AP

Nchini Burundi,uchaguzi wa wabunge umeanza rasmi hii leo baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa mapema asubuhi. Ifahamike kuwa vyama vya upinzani vinaususia uchaguzi huu kwasababu ya malalamiko yao kuwa mipango haijakamilika. Hata hivyo chama tawala cha CNDD-FDD cha Rais Nkurunziza kimewasilisha wagombea wake na ni vyama vidogo vya upinzani vinavyoshiriki katika zoezi hilo.

Uchaguzi huu unafanyika katika mazingira ya hofu baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kutisha kuwa huenda ikaishambulia Burundi kwasababu ya mchango wake katika ujumbe wa Somalia wa kulinda amani.

Ili kupata picha kamili ya jinsi shughuli inavyokwenda Thelma Mwadzaya alizungumza na mwandishi wetu Amida Issa aliyekuwa kwenye kituo kimoja cha kupigia kura mjini Bujumbura. Anaanza kwa kulielezea zoezi lenyewe.