Matangazo
Uchaguzi ambao ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka huu katika Jamhuri ya Kidemokrasai ya Kongo umeahirishwa. Tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo, CENI imesema inatarajia uchaguzi kufanyika Desemba mwaka 2018. Je raia wa Kongo wanasema nini kuhusu uamuzi huo? Je muda wa takriban miaka miwili ulioongezwa utatosha kukamilisha barabara maandalizi kwa ajili ya uchaguzi? Na je mustakabali wa uchaguzi ni upi?