Uchina yaanda mazungumzo ya Korea Kaskazini:
14 Februari 2004Matangazo
SEOUL:
Uchina imeanza kuandaa yale mazungumzo ya
mataifa sita kuhusu programu ya inayoleta
ubishi ya kinyuklea ya Korea ya Kaskazini.
Mazungumzo hayo yamepangwa kufanyika mjini
Beijing hapo Februari 25. Naibu wa Waziri wake
wa Mambo ya Nje Wang Yi, atakayekuwa Mwenye
Kiti wa Mazungumzo hayo, amewasili Korea ya
Kusini kutokea Japan. Baada ya mazungumzo yake
ya mwanzo pamoja na wanasiasa wa ngazi ya juu
wa Korea ya Kusini, Bwana Wang alisema ana
matumaini mema kuwa yatafikiwa mapatano ya
kutegemewa. Lakini ni muhimu juhudi za amani
ziendelezwe juu ya kuweko matatizo, alisema.
Korea ya Kaskazini imesema itayari kuvunja
programu yake ya kinyuklea ikiwa upande wake
Marekani itaipatia tena mafuta na kuondoa
vikwazo vyake vya kiuchumi.