1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi na Ulimwengu wa leo wa biashara – Utajiri unazidi kutiririka

29 Aprili 2011

Bado hatujagundua siri ya kutajirika haraka. Lakini kwa vidokezo kuhusu ulimwengu wa biashara na uchumi na jinsi unavyoweza kufaulu katika ulimwengu wa biashara, sikiliza vipindi vya Noa Bongo Jenga Maisha Yako!

https://p.dw.com/p/NTbc
Wakulima wadogo wadogo na wafanyabiashara ni uti wa mgongo wa uchumi wa AfrikaPicha: DW

Bara la Afrika ni uwanja wa shughuli nyingi za kiuchumi. Kwa mfano ukitazama tu jijini au kijijini mwako, biashara imenoga kila upande. Iwe wauzaji wa nguo kuukuu yaani mitumba, wenye vioski vya kuuza kadi za simu za mkononi au hata vyakula na vinywaji.


Suala jingine ni chimbuko na hali ngumu  inayowakumba wafanyabiashara wa sekta ya juakali. Wafanyabiashara katika sekta hii wanakumbwa na hali ngumu ya maisha kutokana na pato duni, ukosefu wa bima ya afya bila kusahau ukosefu wa bima ya malipo ya uzeeni.


Katika mchezo wa redio wa Noa Bongo kuhusu masuala ya uchumi na biashara, kutana na vijana wawili wanaoamua kujitosa katika ulimwengu wa biashara. Ndugu hawa wawili John na Jane, wote wakiwa na umri wa miaka 16  wanalazimika kugawa muda wao, ili kupata muda wa kuishi na baba yao na bibi yao mzaa mama baada ya kumpoteza mama yao. Siku moja wakiwa likizoni baada ya shule kufungwa, wanaamua kutenga muda kuanzisha biashara. Ungana nao katika safari yao ndefu hadi kufikia kilele cha ufanisi katika shughuli za kibiashara na changamoto wanazokumbana nazo njiani.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako; vinasikika katika lugha sita; Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kireno na Amharic. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani