Rais Felix Tshisekedi ametoa mwito kwa wafuasi wa chama chake wabaki watulivu huku akiahidi kuchukuwa hatua muafaka hii leo baada ya mkutano na viongozi wa taasisi nyingine za kitaifa kufuatia uchaguzi wa seeti uliosababisha machafuko. Chama cha rais mstaafu Joseph Kabila kilinyakuwa asilimia 90 ya viti kwenye uchaguzi huo.