UEFA inaandaa mkutano mkuu Budapest
2 Mei 2016Matangazo
Uongozi wa UEFA utajadili leo miundo ya mashindano, masuala ya kinidhamu na kusikiliza ripoti nyingine muda mfupi kabla ya kuanza dimba la Kombe la Mataifa ya Ulaya Euro 2016 nchini Ufaransa kuanzia Juni 10.
UEFA inataka kudhihirisha kuwa ingali na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua maamuzi katika wakati huu ambapo kuna mgogoro wa uongozi, huku ikisubiri uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo kuhusu Platini. Platini alikata rufaa dhidi ya hatua ya FIFA kumsimamisha kazi na kesi hiyo ikasikilizwa Ijumaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu