PSG na Man City zaondolewa vikwazo na UEFA
4 Julai 2015Matangazo
UEFA imesema imeondoa baadhi ya vikwazo kuhusiana na shughuli za uhamisho wa wachezaji, gharama za wafanyakazi na idadi ya wachezaji wanaoshiriki katika mashindano ya vilabu vya UEFA ambavyo vilikuwa vimewekwa dhidi ya vilabu hivyo viwili mwaka jana.
Shirikisho hilo limesema hatua hiyo imefikiwa baada ya City na PSG kufikia baadhi ya malengo kuelekea katika kuzingaita sheria hizo za utaratibu wa haki za masuala ya kifedha. UEFA haikutoa maelezo zaidi kuhusiana na hilo.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu