1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa yaihimiza ICJ kufafanua sheria juu ya tabianchi

5 Desemba 2024

Ufaransa leo imeihimiza Mahakama ya ICJ kufafanua sheria ya kimataifa inayohusiana na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, ikisema majaji wana fursa maalumu ya kutoa maelezo ya wazi kuhusu mfumo wa kisheria.

https://p.dw.com/p/4nnmE
Uholanzi | ICJ | Nicaragua | Deutschland
Majaji katika mahakama ya ICJ mjini The Hague, Uholanzi, Aprili 9, 2024.Picha: Robin van Lonkhuijsen/ANP/AFP/Getty Images

Ufaransa imeihimiza Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ mjini The Hague, kufafanua sheria ya kimataifa inayohusiana na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, ikisema majaji wana fursa maalumu ya kutoa maelezo ya wazi kuhusu mfumo wa kisheria.

Soma pia: Netanyahu akosoa uamuzi wa ICJ ni "uamuzi wa uwongo"

Mwakilishi wa Ufaransa katika kesi hiyo Diego Costa amesema Ufaransa ina hakika kwamba vikao hivyo vya ushauri vinatoa fursa ya kipekee kwa mahakama kuchangia katika kutambua na kufafanua sheria za kimataifa kuhusu mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuongeza kuwa maoni ya mahakama hiyo ni ya kuaminika.

Ufaransa ni moja ya mataifa na mashirika zaidi ya 100 yanayoshiriki katika vikao hivyo vya mahakama ya ICJ, hii ikiwa kesi kubwa zaidi kuwahi kufikishwa katika mahakama hiyo ya juu duniani.