Uganda: Fred Batale mlemavu anawasaidia walemavu wenzake kujikwamua kiuchumi
18 Novemba 2015
Nchini Uganda watu wenye ulemavu wananyanyapaliwa. Lakini Fred Batale aliuchukua ubaguzi huo kama changamoto. Aliamua kuanzisha mradi wa sanaa kwa walemavu Uganda, akiwa na lengo la kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwapatia maarifa ya sanaa na ubunifu.