1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUingereza

Uingereza yajiunga na ukanda wa biashara wa Indo-Pasifiki

15 Desemba 2024

Uingereza imekuwa taifa la kwanza la Ulaya kujiunga kwenye ukanda mkubwa wa kibiashara wa Indo-Pasifiki.

https://p.dw.com/p/4oAC6
Bendera ya Uingereza
Uingereza yawa taifa la kwanza la Ulaya kujiunga na ushirika wa kibiashara wa Indo-PasifikiPicha: Beata Zawrzel/NurPhoto/picture alliance

Hatua hii ya Uingereza inasifiwa kama mpango mkubwa zaidi wa kibiashara wa taifa hilo, tangu mchakato wa kujiondoa Umoja wa Ulaya - Brexit.

Uingereza sasa inatambulika rasmi kuwa mwanachama wa 12 wa kanda hiyo inayojulikana kama CPTPP, baada ya kutia saini ya kujiunga mwaka uliopita.

Maafisa wanataraji kwamba unachama wa Uingereza utaimarisha uchumi wake kwa hadi pauni bilioni 2.0 kwa mwaka.

Ushirika huo unajumuisha mataifa ya G7, yenye uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni, Canada, Japan, pamoja na washirika wa muda mrefu Australia na New Zealand, Brunei, Chile, Malaysia, Mexico, Peru, Singapore na Vietnam.