Urusi inaendelea kuishambulia Ukraine kwa makombora na droni. Watu wanakimbilia maeneo ya kujificha katika vituo vya treni na katika sehemu ya chini ya majumba yao, kutokana na hilo usalama wa Ujerumani unajadiliwa. Taifa hilo limeanza kuandaa maeneo ya raia kujificha kufuatia kuzidi makali ya mzozo wa Urusi na Ukraine. Je hali ya ulinzi ya Ujerumani ikoje?