1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yashinda, Uholanzi yakwama

10 Juni 2012

Ujerumani ilianza kampeni yake ya kutafuta kombe la UEFA EURO 2012 kwa ushindi muhimu wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Ureno. Nayo Denmark iliiduwaza Uholanzi kwa kuifunga hilo hilo goli moja kwa sifuri.

https://p.dw.com/p/15BTT
Germany's Mario Gomez (2R) scores a goal against Portugal's Rui Patricio during their Group B Euro 2012 soccer match at the new stadium in Lviv, June 9, 2012. REUTERS/Darren Staples (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
EURO 2012 Fußball Deutschland Portugal Gruppe BPicha: Reuters

Ujerumani iliendeleza sifa yake ya kuanza taratibu vinyang'anyiro vikubwa Jumamosi jioni mjini Lviv, Ukraine. Mchezo wa nguvu, wenye mtiririko ambao ulidhihirishwa na Ujerumani katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 2010 nchini Afrika Kusini, kwa mfano, ulikosekana hasa katika kipindi cha kwanza.

Ni kiungo mshambuliaji pekee Mesut Özil ambaye alionekana kuonyesha ubunifu katika safu ya katikati mwa uwanja kwa upande wa kikosi cha Wajerumani.

Bao lake Mario Gomez la dakika ya 72 lilihakikisha mwanzo bora
Bao lake Mario Gomez la dakika ya 72 lilihakikisha mwanzo boraPicha: Getty Images

Lakini wakati Wajerumani wakishjindwa kuonyesha makali, Ureno nayo ilikuwa katika hali hiyo hiyo. Nahodha Cristiano Ronaldo ndiye aliyejaribu tu kuonyesha umahiri wake na kuitatiza Ujerumani, na chanzo kingine cha hatari kilikuwa mchezaji wa ubavuni Nani.

Bao la Ujerumani lilitokea katika dakika ya 72 kwa njia rahisi. Bastian Schweinsteiger alikuwa amenyimwa krosi safi katika upande wa kulia, wakati alipoipokea nje ya kijisanduku. Krosi yake ilimgonga mchezaji wa Ureno Joao Moutinho na Gomez akatia kichwa safi hadi pembeni mwa lango. Ujerumani na Uholanzi sasa zitarejelea uhasimu wao wa jadi mjini Kharkiv siku ya Jumatano.

Kocha wa Uholanzi Bert van Marwijk anasema hawatavunjika moyo. Kwamba ni lazima waizabe Ujerumani.

Uholanzi yaduwazwa

Katika mchauno wa kwanza, Uholanzi ilipoteza nafasi chungu nzima za wazi katika kichapo hicho ambacho hakikutarajiwa. Nyota kama vile Robin van Persi, ambaye ni mfungaji bora wa ligi ya Uingereza, na Arjen Robben ndio waliofanya makosa makubwa wakati timu hiyo iliposhindwa kutumia nafasi 28 za goli walizopata.

Denmark, ambaye ndiye mshindi wa UEFA EURO 1992, ilihitaji tu goli safi lake Michael Krohn-Dehli katika dakika ya 24 na kujiandikishwa ushindi kwenye kundi B.

Arjen Robben hakuamini matokeo baada ya mchuano wao na Denmark kukamilika
Arjen Robben hakuamini matokeo baada ya mchuano wao na Denmark kukamilikaPicha: Reuters

Awali nchini Poland, shirikisho la soka la Urusi lilishitakiwa na shirikisho la UEFA baada ya ukanda wa video kuonyesha mashabiki wa Urusi wakiwashambulia walinzi wa uwanjani baada ya ushindi wa t8imu hiyo wa mabao manne kwa moja dhidi ya Jamhuri ya Czech mjini Wroclaw Ijumaa.

Wafanyakazi wanne wa usalama walitibiwa hospitalini. Jopo la nidhamu la UEFA litaisikiliza kesi hiyo dhidi ya Urusi Jumatano ijayo. Linatafita ushahidi zaidi ili kuchunguza madai ya ubaguzi yaliyofanywa dhidi ya wachezaji wa Czech.

Jumapili (09.06.2012) mabingwa wa Ulaya Uhispania wataanza kulitetea taji lao dhidi ya Italia mjini Gdansk, Poland. Ireland itarejea tena katika dimba hilo baada ya kuwa nje kwa miaka 10, wakati itakapogaragaza na Croatia mjini Poznan katika mchuano mwingine wa kundi C.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Sekione Kitojo