Ujerumani yawashitaki watu watatu kwa njama ya ujasusi
31 Desemba 2024Matangazo
Mshukiwa mkuu Dieter S. anaaminika kwa mwanamgambo mkongwe wa kundi la wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi nchini Ukraine, ambalo Ujerumani inalizingatia kuwa la kigaidi.
Waendesha mashtaka wanasema kwamba lengo kuu lilikuwa ni "kuuhujumu msaada wa kijeshi unaotolewa na Ujerumani kwenda Ukraine kuisaidia katika vita vya uvamizi wa Urusi.
Mashtaka yanasema kuwa Dieter S. alikubali kufanya mashambulizi ya milipuko na ya kuyachoma moto maeneo tofauti nchini Ujerumani. Yanaongeza kuwa mshukiwa huyo aliyachunguza maeneo ambayo ni pamoja na vituo vinavyotumiwa na wanajeshi wa Marekani. Watu wengine wawili wanashukiwa kumsaidia mshukiwa mkuu kupanga njama hiyo. Wote watatu wana uraia wa Ujerumani na Urusi.