1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Kimarekani wazuru kituo cha kinyulea Korea ya Kaskazini:

11 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkM
BEIJING: Ujumbe wa Kimarekani umeitembelea riekta ya kinyuklea ya Korea ya Kaskazini, YONGBON, iliyo kiini cha mgogoro kati ya Washington na Pyongyang. Waliruhusiwa kuvitembelea vituo vyote, kundi hilo la mabingwa liliwaambia waandishi habari mjini Beijing. Habari kamili zitatangazwa baada ya kuarifiwa serikali mjini Washington, walisema mabingwa hao. Pamoja na hayo, walisisitiza kuwa ziara yao haikufanywa rasmi. Baada ya kuondoka ujumbe huo, Shirika Rasmi la Habari la Korea ya Kaskazini, KCNA liliarifu kuwa wageni hao walionyeshwa kiwango cha nguvu za kinyuklea cha nchi hiyo. Serikali ya Marekani imeishutumu mara kadha serikali ya Pyongyang kuwa na niya ya kuunda silaha za kinyuklea.