1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Kimarekani wazuru kituo cha kinyulea Korea ya Kaskazini:

10 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkW
BEIJING: Ujumbe wa Kimarekani umekitembelea kituo cha kinyuklea cha Korea ya Kaskazini, YONGBON, kilicho kiini cha mgogoro kati ya Washington na Pyongyang. Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea ya Kaskazini imeualika ujumbe huo ulioongozwa na watafiti wa kinyulea John Lewis na Sig Hecker na kutekeleza maombi yao yote, ilisemekana ujumbe huo uliporudi mjini Beijing. Lakini taarifa hiyo haikusema kitu chochote kuhusu matokeo ya ziara hiyo. Serikali ya Marekani inaishutumu serikali ya Pyongyang kuwa na niya ya kuunda silaha za kinyuklea. Mgogoro wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili ulianza tena pale Korea ya Kaskazini ilipoifungua upya riekta yake ya kinyuklea huko Yongbon mwaka 2002, baada ya kukifunga mwaka 1994 kufuatana na mawafikiano yaliyofikiwa na Marekani.