SiasaUkraine
Ukraine yafikiria kuhamasisha watu 500,000 wajiunge na jeshi
20 Desemba 2023Matangazo
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameuambia mkutano wake wa mwisho wa mwaka na waandishi wa habari kwamba, suala hilo ni "nyeti" na kwamba jeshi na baraza lake la mawaziri litajadiliana kwa kina kabla ya kuamua kuwasilisha pendekezo hilo bungeni.
Zelenskiy ameongeza kuwa anahitaji kufanyike majadiliano zaidi juu ya pendekezo la kuongeza watu zaidi jeshini kabla ya hatimaye kuliunga mkono.
Idadi kamili ya wanajeshi wa Ukraine haijulikani, ila inasadikika kuwa karibu watu milioni 1 nchini humo wamepokea mafunzo ya kutumia silaha.
Urusi imekuwa ikitanua kwa kasi jeshi lake wakati wa vita na Ukraine na ilieleza jana kuwa inapanga kuongeza askari wake hadi milioni 1.5.