Ukraine yaashiria kuhusika na mauaji ya Kirillov
17 Desemba 2024Matangazo
Shirika la habari la Urusi, Interfax, na mashirika mengine ya habari yamezinukuu duru ndani ya SBU zikithibitisha kuhusika na mauaji ya jenerali huyo. Duru hizo za SBU zimesema Jenerali Kirillov alikuwa muhalifu na amekuwa akilengwa kwa madai ya kuamuru matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya wanajeshi wa Ukraine katika uwanja wa mapambano. Uingereza na Marekani ziliwahi kuishutumu Urusi kutumia sumu aina ya chloropicrin dhidi ya wanajeshi wa Ukraine kinyume na Mkataba wa Silaha za Kemikali. Urusi imekanusha tuhuma hizo na kusema haimiliki tena aina hiyo ya silaha za kemikali.