1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Raia wetu takriban 13,500 wamerejea kutoka Urusi

24 Novemba 2023

Mamlaka za Ukraine zimefahamisha hii leo kuwa raia wake zaidi ya 13,500 wamerejea nchini humo wakitumia njia pekee inayopakana na Urusi ambayo ilifunguliwa majira ya joto.

https://p.dw.com/p/4ZQOy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: president.gov.ua

Raia hao wameingia kupitia eneo la Summy mashariki mwa Ukraine na idadi hiyo inawajumuisha watoto 1,653 na watu 131 wenye ulemavu. Moscow imeshutumiwa mara kadhaa kwa kuwahamisha kwa nguvu maelfu ya raia wa Ukraine hadi nchini Urusi.

Kyiv inasema imeorodhesha takriban watoto 20,000 ambao walipelekwa Urusi baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake nchini humo Februari mwaka jana.

Soma pia: Urusi yaendeleza mashambulizi mashariki mwa Ukraine

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ilitoa mwaka huu waranti wa kukamatwa rais Vladimir Putin kutokana na harakati haramuya kuwahamisha watoto kutoka katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.