Ukraine yasema wanajeshi wengi wa Korea Kaskazini wameuawa
18 Desemba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa mazungumzo ya simu yaliyorekodiwa kwa njia ya siri, shirika la ujasusi la Ukraine SBU limeeleza kuwa zaidi ya askari 200 wa Korea Kaskazini waliojeruhiwa wamelazwa hospitali karibu na mji mkuu Moscow.
Hata hivyo taarifa hizo za SBU hazikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pia amegusia mara kadhaa kuhusu kuuliwa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika siku za hivi karibuni.
Zelensky pia ameishtumu Urusi kwa kuchoma maiti za wanajeshi waliouawa vitani ili kuficha idadi kamili ya vifo.