SiasaUkraine
Ukraine yathibitisha kutumia makombora ya ATACMS
18 Oktoba 2023Matangazo
Ukraine ilitumia makombora hayo yaitwayo ATACMS kushambulia kambi mbili za jeshi la angani jana Jumanne katika eneo linalokaliwa na Urusi.
Vikosi vya operesheni maalum vya Ukraine vilisema shambulizi la Jumanne liliharibu njia za ndege, helikopta tisa, ghala la risasi, kirusha makombora ya kudungua ndege na vifaa vingine vya kijeshi.
Hata hivyo madai hayo hayakuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.
Ukraine ilipewa makombora hayo na Marekani, wakati ilikuwa ikijitahidi kujibu mashambulizi kusini na mashariki mwa nchi yake.
Uamuzi huo ulioashiria mabadiliko ya msimamo wa utawala wa Rais Joe Biden.