Marais wa nchi za Umoja wa Afrika wajadiliana kufadhili miradi ya maendeleo ya umoja huo, tatizo la uhamiaji na ufumbuzi wa migogoro kwenye nchi kadhaa. Mwenyeketi mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema bila mshikamano maendeleo ni ndoto Afrika, huku mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Rais Alpha Conde wa Guinea, akisema kuwa matatizo ya Afrika yatatuliwe na Waafrika wenyewe.